Tuesday, October 19, 2010

Spear Mbwembwe na Eliud Pemba wakiwakilisha vyema na Kilimanjaro Beer huku Godfrey akimpa ushauri Danny Mrwanda kwa mbali.
wataalamu wa soka wakiwa wanapewa maelekezo na mwalimu edwin wandawanda hapa anaonekana diego, haule, katembo othman, herry Kisiki, Mussa Stam na salum wakati wa nanenane morogoro 2010
Leonard Richard (Ghetto) akipokea zawadi yake baada ya kuchaguliwa mchezaji bora katika mchezo wa soka baina ya Segerea Veterans na Tanzania Stars wakati wa bonanza la nanenane jamhuri morogoro.

Professor Madundo Mtambo mwanasoka msomi aliyetukuka akikabidhiwa zawadi yake ya mwanasoka bora katika mchezo baina ya SUA Veterans na Kisukulu, zawadi zilitolewa na Mratibu wa bonanza la nanenane 2010 uwanja wa Jamhuri Morogoro.

wakuu wa hat-trick, leonard Richard na Diego Mohamed wakiwa pamoja na Majugwa na Mhe: Ally Katembo muda mfupi kabla ya kukwea pipa kuelekea morogoro wakati wa sherehe za nanenane 2010.

Monday, October 18, 2010

Gaydon Mtenga, Captain Fantastic John Nyemo, Leonard Mwakasege, mohamed Diego na Godfrey wakijiuliza ni kwa jinsi gani wameweza kupata mabilioni ya kuwekeza eneo la ekari mia tano ambalo timu ya Segerea Veterans wanamiliki huko Maneromango.
Mwalimu Spear Mbwembwe akishuhudia makabidhiano ya vifaa vya michezo baina ya Edwin Wandawanda kiongozi wa Segerea Veterans na Bwana shaibu kiongozi wa Maneromango Combain huku Leonard Richard na salum Mwamtuya wakiaangalia kwa makini.
Mkurugenzi wa Ibra Construction Ltd na Maderaine Clearing and Forwarding Bwana Emmanuel Kazimoto (kushoto )ambaye pia ni mmiliki wa timu ya Segerea Rangers akiwa na kipaji kipya ambacho kinasemekana kuwa ata kocha wa vijana Tinnicko alipokwenda na Kocha maximo walikitambua na watu wakambania mtoto huyu. Huyu mtoto ni balaa, yaani ni kama Tevez anaitwa Kassimu na kwao ni maarufu kama Daniel Alvez. tegeni masikio juu ya dogo huyu.
Salum Mwantuya, Wandawanda na Anwar Awadh wakiwa na viongozi wa Maneromango Combain muda mfupi baada ya kuwakabidhi vifaa vya michezo, jezi, tracksuit, mipira na nyavu timu ya Segerea Veterans imeonesha mfano wa kuigwa huko Maneromango
Aksanteni washabiki wetu, maana bila ya nyinyi sijui ingekwaje?
Rashid Idd Chama, Anwar Awadh" Kaito' na Masoud Rehani wakiwa wamepozi baada ya mazoezi makali na timu ya Segerea Veterans

Sunday, October 17, 2010

Kwa swagger mgogo huyu! khaaa. yaani uatfikiri sio mpwa wake matonya
Gaydon Mtenga akiangalia eneo ambalo Segerea Veterans imenunua kiasi cha ekari mia tano maeneo ya Kikwete kuelekea Maneromango
Alex, Witness na Emmanuel Kazimoto ndani ya Maneromango wiki end ya jana 17/10/2010
Je unamkumbuka huyu? si mwingine ni Rshid Idd Chamaakivinjari na Segerea Veterans ana kuahidi kuwa kila wakati akifika Dar es salaam atakuwa ni mgeni wa Segerea Veterans.
Beki mahiri wa zamani wa Yanga Africans Anwar Awadh "Kaito" akipasha na timu yake mpya ya Segerea Veterans

Saturday, October 9, 2010

Monday, August 16, 2010


Mwalimu Spear Mbwembwe akiongoza sebene la Twanga pepeta huku wachezaji wake wa segerea veterans Aleche Ninje, Emmanuel Kazimoto, Leonard Richard na Othman Katembo wakiserebuka kwa chati uwanja wa Jamhuri Morogoro wakati wa tamasha la nanenane kabla ya kupambana na Tanzania Stars chini ya Juma Mkambi 'General'
Wajumbe wa kamati ya fitna Edwin Wandawanda, Andrew Ng'ong'a, Ally Ruvu, Garfield Haule, Yakub Matula na Othman Katembo wakati wa nanenane Morogoro 2010. Masuka Village

Friday, June 18, 2010

Gaydon Mtenga na Yackub Matula wakijadiliana na Jerryson Tegete ni kiasi gani atawaachia Segerea Veterans atakapouzwa nchini Sweden maana mgao sio Yanga peke yao ata sie tume, tunamchaji kimazoezi na kumpa vitu adimu kila jumamosi na jumapili.
huyu mtu muhimu saana wakati wa asubuhi baada ya mazoezi, almaarufu kama mama uji., ana bonge la mwanya wa juu.

Khalid Oming'o akijidai na kombe la uji. kushoto ni yule beki maridadi wa Yanga Anwar Awadh akiwa na mwanae pamoja na Salum Mwamtuya na Rogers Mwakalukwa wakijipumzisha baada ya mazoezi.

Monday, May 24, 2010



"the Special One" kutua Segerea Veterans.

Homa imeanza kuwapanda waalimu ya timu ya Segerea Veterans kuwa yule kocha mwenye mafanikio na mbwembwe nyingi kipenzi cha watu, kiboko wa wote wenye akili Jose Mourinho yupo mbioni kukamilisha mkataba wa siku kumi kukinoa kikosi hicho. aaaaaaaahhh, utani tu jamani.

Mipango ya msosi ikiandaliwa hapa wakuuwa Segerea Veterans wakapata maelezo ya kina toka kwa mkuu wa mambo ya misosi bwani Mujuni.
Viongozi wa Mbeya Veterans Ndalo na viongozi wa Segerea Veterans Mh; Ally Katembo na Wetson Mwamafupa wakimsikiliza Mh: Magungu hayupo pichani wakati wa nasaha.
Katibu Mkuu Kiongozi Ofisi ya Segerea Veterans Mh: Wetson Mwamafupa akitoa nasaha zake kwa wageni wetu wa Mbeya Veterans (Mbalizi) wakati wa pasaka 2010.
Mwenyekiti wa Segerea Veterans Mh: Magungu akishiriki chakula pamoja na timu zote shiriki katika bonanza la mwaka 2010 wakati wa pasaka na kuhudhuriwa na timu tatu, wenyeji segerea , Mbeya Veterans na Buguruni Veterans.
"Huyu mama mpishi vipi? yaani nyama anawapa wengine wakati mie kanipa wali mtupu" hapa anaonekana mchezaji Nyemo John Chinyabe akiwaza kwa mshangao. wagogo kwa nyama!!
Leonard Richard, Shaabani Machumane na Wetson Mwamafupa wakisikiliza maneno ya busara kutoka kwa wawakilishi wa Mbeya Veterans baada ya kumalizika kwa mchezo kirafiki baina yao wakati wa sherehe za pasaka 2010.
Vikosi mchanganyiko Mbeya Veterans na Segerea Veterans wakati wa bananza la pasaka 2010 huko segerea dar es salaam
beki Ayawi Daraja akitafuta namna ya kupiga chenga shambuliaji moja la Buguruni, bonge la mtu. ngoja tutamuuliza kama alifanikiwa kupiga chenga.
Anaitwa Haule beki wa Segerea Veterans akianua kinu juani kuepuka lawama dhidi ya wachezaji watatu wa Buguruni Veterans wakati wa bonanza segerea wakati wa pasaka 2010.
wanamwita Ngassa wa Segerea Veterans, hapa Mh: Ally Katembo akimnyanyasa beki wa Mbeya Veterans kwa chenga za maudhi na kutoa pasi kama za Gaucho.

Hatuna hakika kama hapa Kibona alipitwa ama laa. Kwani huyu jamaa labda upite mpira peke yake ama mchezaji peke yake, kupita vyote ni ngumu sana. wanaume kazini Segerea Veterans na Buguruni Veterans wakati wa Pasaka 2010.
Timu kamambe ya Mbeya Veterans (Mbalizi) baadhi ya wachezaji ni kama Shaaban kiungo wa zamani wa Majimaji wapili kushto waliosimama na Ephraim Kayeta mshambuliaji mwenye akili, kasi na mashuti wa timu za Mecco ya Mbeya na timu ya taifa ya tTanzania enzi hizokatikati waliosimama. hapa ni kabla ya pambano lao na timu ya Buguruni Veterans wakati wa pasaka 2010. Wengine pichani ni jairo, mwasa, kaunda na wengineo.
Kutoka kushoto waliosimama ni Mwalimu Wandawanda, Karume Uledi, Gaydon Mtenga, Mganga Laurian, Khalid Oming'o, Shaaban Machumane, Ayawi Ally Daraja, Ephraim Makoye, Mao Mkami (Ball Dancer) Mh: Ramadhani Maleta, Airform Kibona,Muhidini Sisso na Spear Mbwembwe. Waliochuchumaa kutoka kushoto ni Nyemo John Chinyabe (Berbatov) Leonard Richard Mwakasege (Zidane) Mohameid "Kukovic" Mh: Ally Katembo, Mohameid Diego, Salum Mwamtuya (Baba Said) na Eliud Pemba. Hiki ndio kikosi kamili cha Segerea Veterans kilichopambana na timu za Mbalizi Veterans na Buguruni Veterans wakati wa sherehe za pasaka 2010.
Kutoka kushoto Mh: Ally Katembo, Khalid Oming'o, Mh: Ramadhani Maleta, Gaydon Mtenga,Mganga Laurian na Muhidini Sisso wakipasha kuwakabili Buguruni Veterans siku ya PASAKA 6/4/2010
Baadhi ya wachezaji wa Mbalizi Veterans kutoka Mbeya wakipiga jaramba kabla ya kuikabili timu ya Segerea Veterans

Friday, April 9, 2010

Mratibu wa mashindano ya Mashujaa Bonanza na ambaye pia ni kocha mkuu wa Segerea Veterans Spear Dunia Mbwembwe akaingalia wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa uongozi wa timu ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars hivi karibuni katika uwanja wa magereza Ukonga.

Monday, March 22, 2010

TANZIA

Uongozi na wanachama wa Segerea Veterans Sports Club wanasikitika kutangaza kifo cha mwanachama mwenzao wa Hiyari ambaye pia ni mke mkubwa wa Senior Member Chief Uyeka Idd Lumbyambya Mavanga wa pili kilichotokea siku ya jumamosi tarehe 20/3/2010 na mazishi kufanyika siku hiyo hiyo katika makaburi ya Kichifu huko Segerea. (Innah hillah Raajun)

Tulimpenda saana shemeji yetu, lakini Allah amempenda zaidi. Amin.

Tuesday, February 23, 2010

Timu ya Segerea Veterans siku ya jumapili tarehe 21/02/2010 ilitoa dozi kali kwa timu ya Buguruni Combine Veterans kwa kipigo cha magoli 3-2 magoli yakiwa yamewekwa kimiani na Airform Kibona (penati dk ya 15), Ally Ruvu mchezaji wa zamani wa timu za Simba Sports Club na JKT Ruvu na Karume (Mmanyema). Nyota ya mchezo alikuwa ni Mao Mkami (Ball Dancer) mkali wa zamani watimu za TP Lindanda Pamba (wana kawekamo) ya Mwanza na timu za Mtibwa na Manyema. Jamaa huwezi amini, yupo sawa kama alivyo kuwa enzi hizo akiwalisha mipira kina Fumo Felician, Kitwana Selemani, Beya Simba, Hussein Marsha na wakali wengine wa TP Lindanda. Still dancing with a ball as he was doing decades ago, bravo pal.

Saturday, February 13, 2010

Jamaa wa Boko sio mchezo, siunaona Mwalimu wa Segerea Veterans anashindwa hata kujua hii ni aina gani ya bia. Bahati mbaya ata Ayawi pia hajui aina ya bia maana yeye Hanywi pombe. wale wengine maskini wanaangalia nini sijui.
Mheshimiwa Ally Katembo akichangia mawaidha ya busara na Ndugu zetu wa Boko Veterans. Jamaa walimwaga unywaji si mchezo, hapa anaonekana Mheshimiwa Boli Zozo akikubaliana na mawazo ya Mheshimiwa Katembo kwa kutikisa chupa ya ulabu, wengine pichani ni Muhudini Sisso, Spear Mbwembwe na Juma Katembo mwenye chupa ya maji Uhai.
Beki aliyerudi katika kiwango cha zamani ambaye alikuwa nyota ya Tabora na watu kama Ally Mayai, Huruna Moshi, Idd Moshi, Mrisho Moshi, Mohamed Banka, Yahya Akilimali walikuwa wanajifunza mavitu kutoka kwake Salum Mwamtuya (Baba Said).

Tunatamani kama angekuwa bado anacheza soka ya upinzani labda angeweza kutupa miaka ya sasa. Ukitaka kuona vitu vyake watafute Segerea Veterans wanapocheza, haiitaji kuambiwa utaona beki akiwanyanyasa washambuliaji utajua tu huyo ndiye Salum Mwantuya.
Washkaji wa Boko Veterans wakishauriana jinsi ya kukabiliana na moto wa Segerea Veterans, uongo washkaji wapo sawa kwani mechi iliisha 0-0 ingawa Segerea Veterans walikuwa kamili chini ya kocha Spear Mbwembwe, lakini Boko Veterans chini ya Bekar (Bekar Ranger) walitoa upinzani mzuri.

Wednesday, February 10, 2010



Hawa jamaa wa Ivory Coast bwana noma, si unaona jamaa anavyokojoa, sasa sisi Segerea Veterans tulipokataa kucheza nao watu wakaanza kuchonga kuwa tunaringa sababu ya kiwango chetu, ukweli ni kuwa uwanja wetu ni msafi tunaogopa jamaa wangechafua.

Monday, February 8, 2010

jana jumapili tarehe 6/2/2010 timu kabambe ya Segerea Veterans ilikuwa na mpambano wa kirafiki baina yake na timu machachari ya Mbezi Beach Veterens iliyo chini ya ufadhili na udhamini wa Giraffe Hotel.

Katika mchezo huo matokeo yalikuwa Segerea Veterans 2 na Mbezi Beach Veterans 1 (SVSC 2- MBVSC 1) magoli ya Segerea yaliwekwa kimiani na mchezaji wa zamani wa simba na yanga Ephraim Makoye katika dakika ya 7 na Karume dakika ya 30 kipindi cha pili na lile la Mbezi Beach liliwekwa kimiani na mchezaji wa zamani wa Ushirika Moshi Hashimu. (picha zitafuata baadae)

Timu ya Segerea ilicheza mchezo wa kufurahisha kiasi cha kuwaduwaza wapinzani wao muda wote wa mchezo. Kiungo mahili wa Taifa stars na mchezaji wa timu za Vijana Ilala (Kabaka yeka) na Mtibwa Sugar Hussin Sweddy aling'arisha vilivyo katikati, huku Zidane (Richard) akiikosesha timu yake ya Segerea Veterans magoli kadhaa ya wazi. Nyota ya mchezo kwa mujibu wa Mbezi Beach Veterans alikuwa ni mlinda mlango wa Segerea Veterans Mustafa "Kukovic"


Katika hatua nyingine Timu za Segerea Veterans na Mbezi Beach zinajiandaa kuipokea timu ya Mbeya Veterans siku ya jumamosi ya Pasaka na PASAKA KUU katika mabonanza yatakayo fanyika Mbzi Beach na Segerea. Timu ya Mbeya inayoundwa na wakali wa timu za Tukuyu Stars (Banyambala) na Mecco chini ya uongozi wakali kama charles Makwaza, na wengineo inatarajiwa kuwasili jijini siku ya ijumaa kuu.

Taarifa zaidi juu ya timu za Iringa na Ruvuma zitatolewa hapo baadae.

Thursday, January 28, 2010

Spear Dunia Suleinman Mbwembwe Kocha mkuu wa Segerea Veterans akiwa kazini uwanja wa Jamhuri Morogoro. Pamoja na kuwa kocha pia ni mfanya biashara maarufu wa vifaa makini vya michezo nchini.
REMINISCING on this eventful day; a couple of years (2008) when Segerea Veterans Sports Club hosted a Bonanza in fond memories of their slain President Mperemba (Le Presider). Captured in the photo is Segerea Veterans Chairman Mr. Magungu who happened to be the Guest of Honour presenting a pair of jersey to Leonard Richard (Zidane) after his team emerged overall winners of the tournament. Looking on are Mr. Paul Kidubo and Khalid Oming'o. The ocassion was professionally conducted and administered by Mr. Whatson Mwamafupa and Eliud Pemba.
Siku ya kumbukumbu ya Rais wetu Marehemu Mperemba tuliandaa bonge la mechi za bonanza, hapa Zidane (Richard) akiongoza msafara wa wangoni na wapogoro, yaani haule, Ayawi na Katembo kusalimiana na waungwana wa kina Shafii wa Tabata Kimanga Veterans.
, Mashaka, Haule Toleo la vikosi mbalimbali vya Segerea Veterans, hapa ni siku ya kumbukumbu ya Rais wetu marehemu Mperemba. Kutoka kushto waliosimama ni Martin Richard Tupilike, Bilary, Andrew Ng'ong'a (Nigeria) Chifu Uyeka Idd Lumbyambya Mavanga wa II (Chifu wa Wanyiha na makabila yote madgo mkoa wa Mbeya), Richard Mwakasege (Zidane) na Gaydon Mtenga.
Waliinama kutoka kushoto ni Othman Katembo, Emmanuel Kazimoto (Baba Glory- mkwe) Airform Kibona, Mashaka, Haule, Herry Kisiki, Godfrey na Ernest.
Wazee wa Segerea Veterans kutoka kushoto waliosimama Whatson Mwamafupa, Othman Katembo, Muhdin Sisso, Gaydon Mtenga, Leonard Richard Mwakasege, Khalid Oming'o, Ernest, Macho, Nyemo John Chinyabe, Andrew Ng'ong'a (Nigeria), Chifu Uyeka Idd Lumbyambya Mavanga wa II, Hope Kaizer, na Eliud Pemba (Oyaa Msela Oyaa).
Waliopiga goti toka kushoto ni Bilary,Karume,Babu Ayawi, Herry Kisiki, Mashaka, Airform Kibona na Yackub (Cisse) aliyelala ni Godfrey.