Tuesday, October 19, 2010

Spear Mbwembwe na Eliud Pemba wakiwakilisha vyema na Kilimanjaro Beer huku Godfrey akimpa ushauri Danny Mrwanda kwa mbali.
wataalamu wa soka wakiwa wanapewa maelekezo na mwalimu edwin wandawanda hapa anaonekana diego, haule, katembo othman, herry Kisiki, Mussa Stam na salum wakati wa nanenane morogoro 2010
Leonard Richard (Ghetto) akipokea zawadi yake baada ya kuchaguliwa mchezaji bora katika mchezo wa soka baina ya Segerea Veterans na Tanzania Stars wakati wa bonanza la nanenane jamhuri morogoro.

Professor Madundo Mtambo mwanasoka msomi aliyetukuka akikabidhiwa zawadi yake ya mwanasoka bora katika mchezo baina ya SUA Veterans na Kisukulu, zawadi zilitolewa na Mratibu wa bonanza la nanenane 2010 uwanja wa Jamhuri Morogoro.

wakuu wa hat-trick, leonard Richard na Diego Mohamed wakiwa pamoja na Majugwa na Mhe: Ally Katembo muda mfupi kabla ya kukwea pipa kuelekea morogoro wakati wa sherehe za nanenane 2010.

Monday, October 18, 2010

Gaydon Mtenga, Captain Fantastic John Nyemo, Leonard Mwakasege, mohamed Diego na Godfrey wakijiuliza ni kwa jinsi gani wameweza kupata mabilioni ya kuwekeza eneo la ekari mia tano ambalo timu ya Segerea Veterans wanamiliki huko Maneromango.
Mwalimu Spear Mbwembwe akishuhudia makabidhiano ya vifaa vya michezo baina ya Edwin Wandawanda kiongozi wa Segerea Veterans na Bwana shaibu kiongozi wa Maneromango Combain huku Leonard Richard na salum Mwamtuya wakiaangalia kwa makini.
Mkurugenzi wa Ibra Construction Ltd na Maderaine Clearing and Forwarding Bwana Emmanuel Kazimoto (kushoto )ambaye pia ni mmiliki wa timu ya Segerea Rangers akiwa na kipaji kipya ambacho kinasemekana kuwa ata kocha wa vijana Tinnicko alipokwenda na Kocha maximo walikitambua na watu wakambania mtoto huyu. Huyu mtoto ni balaa, yaani ni kama Tevez anaitwa Kassimu na kwao ni maarufu kama Daniel Alvez. tegeni masikio juu ya dogo huyu.
Salum Mwantuya, Wandawanda na Anwar Awadh wakiwa na viongozi wa Maneromango Combain muda mfupi baada ya kuwakabidhi vifaa vya michezo, jezi, tracksuit, mipira na nyavu timu ya Segerea Veterans imeonesha mfano wa kuigwa huko Maneromango
Aksanteni washabiki wetu, maana bila ya nyinyi sijui ingekwaje?
Rashid Idd Chama, Anwar Awadh" Kaito' na Masoud Rehani wakiwa wamepozi baada ya mazoezi makali na timu ya Segerea Veterans

Sunday, October 17, 2010

Kwa swagger mgogo huyu! khaaa. yaani uatfikiri sio mpwa wake matonya
Gaydon Mtenga akiangalia eneo ambalo Segerea Veterans imenunua kiasi cha ekari mia tano maeneo ya Kikwete kuelekea Maneromango
Alex, Witness na Emmanuel Kazimoto ndani ya Maneromango wiki end ya jana 17/10/2010
Je unamkumbuka huyu? si mwingine ni Rshid Idd Chamaakivinjari na Segerea Veterans ana kuahidi kuwa kila wakati akifika Dar es salaam atakuwa ni mgeni wa Segerea Veterans.
Beki mahiri wa zamani wa Yanga Africans Anwar Awadh "Kaito" akipasha na timu yake mpya ya Segerea Veterans

Saturday, October 9, 2010