Thursday, January 28, 2010

Spear Dunia Suleinman Mbwembwe Kocha mkuu wa Segerea Veterans akiwa kazini uwanja wa Jamhuri Morogoro. Pamoja na kuwa kocha pia ni mfanya biashara maarufu wa vifaa makini vya michezo nchini.
REMINISCING on this eventful day; a couple of years (2008) when Segerea Veterans Sports Club hosted a Bonanza in fond memories of their slain President Mperemba (Le Presider). Captured in the photo is Segerea Veterans Chairman Mr. Magungu who happened to be the Guest of Honour presenting a pair of jersey to Leonard Richard (Zidane) after his team emerged overall winners of the tournament. Looking on are Mr. Paul Kidubo and Khalid Oming'o. The ocassion was professionally conducted and administered by Mr. Whatson Mwamafupa and Eliud Pemba.
Siku ya kumbukumbu ya Rais wetu Marehemu Mperemba tuliandaa bonge la mechi za bonanza, hapa Zidane (Richard) akiongoza msafara wa wangoni na wapogoro, yaani haule, Ayawi na Katembo kusalimiana na waungwana wa kina Shafii wa Tabata Kimanga Veterans.
, Mashaka, Haule Toleo la vikosi mbalimbali vya Segerea Veterans, hapa ni siku ya kumbukumbu ya Rais wetu marehemu Mperemba. Kutoka kushto waliosimama ni Martin Richard Tupilike, Bilary, Andrew Ng'ong'a (Nigeria) Chifu Uyeka Idd Lumbyambya Mavanga wa II (Chifu wa Wanyiha na makabila yote madgo mkoa wa Mbeya), Richard Mwakasege (Zidane) na Gaydon Mtenga.
Waliinama kutoka kushoto ni Othman Katembo, Emmanuel Kazimoto (Baba Glory- mkwe) Airform Kibona, Mashaka, Haule, Herry Kisiki, Godfrey na Ernest.
Wazee wa Segerea Veterans kutoka kushoto waliosimama Whatson Mwamafupa, Othman Katembo, Muhdin Sisso, Gaydon Mtenga, Leonard Richard Mwakasege, Khalid Oming'o, Ernest, Macho, Nyemo John Chinyabe, Andrew Ng'ong'a (Nigeria), Chifu Uyeka Idd Lumbyambya Mavanga wa II, Hope Kaizer, na Eliud Pemba (Oyaa Msela Oyaa).
Waliopiga goti toka kushoto ni Bilary,Karume,Babu Ayawi, Herry Kisiki, Mashaka, Airform Kibona na Yackub (Cisse) aliyelala ni Godfrey.

Thursday, January 21, 2010

Kocha Mkuu wa Segerea Veterans, golikipa mahili wa club za Lipuli, simba na malindi ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu wa vifaa vya michezo Spear Dunia Suleiman Mbwembwe akiteta jambo na mfadhili wa mashindano ya OK Plastic Vingunguti

Wednesday, January 20, 2010

Wanaume Yanga Fans Segerea Veterans mawindoni kumnyatia simba jike. kutoka kushoto ni Mhe: Ally Katembo, Gaydon Mtenga, Karume (mfalme wa waha na watu wote wasio na uhakika na nchi wanazotoka), Leonard Richard (Zidane) pamoja na Andrew Ngong'a (a.k.a Nigeria) wakifanya mawindo kabla ya kuwakabili Simba Fans Segerea Veterans.
Chifu Oyeka Idd Lumbyambya wa II akiwa anajaribu kumuelewa kocha mkuu Wandawanda 9hayupo pichani0 maana hii kichwa ya kinyia inapata taabu saana kuwaelewa hawa wapogoro wa mtimbila na malinyi.
ukiona mtu mzima amejishika miguu ujue kachoka ile mbaya. Timu meneja Gaydon Mtenga aliona kuwa ligwaride limekuwa zito akataka kuchojoa magwanda na kukimbia kazi, si mchezo soka ya uzeeni ina raha na kuchoka, ilibidi Mheshimiwa Katembo afanye kazi ya ziada kumshawishi Mtenga kurejea na kuiongoza Yanga Fans Segerea Veterans kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya mahasimu wao wakubwa Simba Fans Segerea Veterans,. Zidane na Alex wao wanacheka tuu, yaani raaha, utamu.
Chifu wa Wanyia na makabila yote madogo ya Mkoa wa Mbeya Chifu Oyeka Idd Lumbyambya wa II alisimamia vyema mambo yetu ya kula na kunywa, hapa anatamani sijui ampele nani sahani, maana machifu wa aina kwa msosi mhhh.
Mheshimiwa Magungu alikuwawepo kutoa zawadi za ushindi kwa timu mbalimbali ambapo Segerea Rangers timu inayofadhiliwawa na kampuni kubwa ya ujenzi ya Ibra Construction Limited chini ya Mkurugenzi Mkuu Emmanuel Kazimoto na uratibu wa Segerea Veterans.
Kaptain Ommy G (Omary) wa timu ya vijana Segerea Rangers akinyanyua juu kwa furaha seti ya jezi iliyotolewa na mfadhili wa mashindano ya soka kwa vijana Heko Plastic Industries Vingunguti chini ya uratibu wa Spear Mbwembwe na Mohameid Diego.
Bonge la uwanja wa world cup 2010 linaitwa Mbombela Municipal Stadium lipo Nelspruit (Nelcity) South Africa, hapo ilikuwa mwaka jana 2009 mwezi februari. Nasikia tayari limekwisha kamilika. Segerea Veterans tumepewa mwaliko na jamaa wa Valencia Sporting Club Nelspruit kufanya ziara baada ya kwisha kwa world cup 2010. Kila mtu passport juu.
Chifu Oyoka Idd Lumbyambya wa II linapokuja suala la kula mhhhhhhhh! utamtaka? hapa anajaribu kumlaghai Chifu Magungu wa Malinyi kuwa kiutamaduni yeye ndiye anastahili kugawa wale mbuzi waliochinjwa na Nyemo ambapo kocha Mkuu Spear Suleiman Dunia Mbwembwe alifadhili na mheshimiwa Magungu kulipia gharama zote za manunuzi.
hapa nyumba ya fedha (Emmanuel Kazimoto) aliamua kunywa maji yote wengine ikabidi tuwe tunaangalia chini, maana huko mpunga ruvu darajani maji ya kunywa ilikuwa ishu, hasa baada ya Ayawi kutishiwa na bibi mwenye miembe kuwa tukiondoka salama itakuwa ni bahati yetu.
tukikosa safari za mikoani ama ulaya hata Ruvu darajani sie tunakwenda tu. Hapa tupo ruvu darajani tunawakilisha soka la kibongo. usipime ushindi hata kwa wasiojua ni kama jadi yetu segerea veterans. Kapteni Richard (Zidane) na golikipa namba moja Godfrey wakishuhudia refa akipewa rushwa ili jamaa wa mpunga washinde.
Linapokuja suala la uongozi ni mtu kamilifu kiakili, kimwili na kimaadili anapewa nafasi, hapa Mheshimiwa Mwenyekiti Magungu akihakikisha kuwa mchinja nyama maarufu toka DODOMA Nyemo John Chinyabe haondoki hata na kipande cha mbuzi wetu.
Mkurugenzi wa fedha na mambo ya maana Emmanuel Kazimoto (a.k.a Baba Glory) kwa furaha kabisa akicheka baada ya kudanganywa na Mwenyekiti wa kamati ya ufundi Diego Mohameid kuwa Simba Fans segera watashinda dhidi ya Yanga fans segerea, duuh wala haikuwa hivyo wazee walichezea mbili moja kama kawaida siku ya jumapili tarehe 03/01/2010 kwa magoli ya Karume na Alex kutokana na kazi nzito ya Richard (Zidane)
Mh; Ally Katembo, Leonard Richkard, yackub (a.k.a.)Cisse na Salum (Baba Said) wakijiandaa kuwamaliza Simba Sports Club Fans kwenye uwanja wa Emirates Segerea toto tundu.
DUUH. ningejua kuwa vifaa hivi bongo ni bei kubwa kihivi si ningebeba kwa madiba nije niwabane wazee wangu wa vitambi segerea kin Mheshimiwa Katembo, chifu Oyoka na kina Emma Kazimoto, safari ijayo lazima niwanunulie mzigo.
siku mwanablogger wa segerea veterans Leonard Richard a.k.a. Ghetto B kulia alipoa amua kuachana na mambo ya Nyemo (kuwa bachela mkongwe)