Monday, May 24, 2010



"the Special One" kutua Segerea Veterans.

Homa imeanza kuwapanda waalimu ya timu ya Segerea Veterans kuwa yule kocha mwenye mafanikio na mbwembwe nyingi kipenzi cha watu, kiboko wa wote wenye akili Jose Mourinho yupo mbioni kukamilisha mkataba wa siku kumi kukinoa kikosi hicho. aaaaaaaahhh, utani tu jamani.

Mipango ya msosi ikiandaliwa hapa wakuuwa Segerea Veterans wakapata maelezo ya kina toka kwa mkuu wa mambo ya misosi bwani Mujuni.
Viongozi wa Mbeya Veterans Ndalo na viongozi wa Segerea Veterans Mh; Ally Katembo na Wetson Mwamafupa wakimsikiliza Mh: Magungu hayupo pichani wakati wa nasaha.
Katibu Mkuu Kiongozi Ofisi ya Segerea Veterans Mh: Wetson Mwamafupa akitoa nasaha zake kwa wageni wetu wa Mbeya Veterans (Mbalizi) wakati wa pasaka 2010.
Mwenyekiti wa Segerea Veterans Mh: Magungu akishiriki chakula pamoja na timu zote shiriki katika bonanza la mwaka 2010 wakati wa pasaka na kuhudhuriwa na timu tatu, wenyeji segerea , Mbeya Veterans na Buguruni Veterans.
"Huyu mama mpishi vipi? yaani nyama anawapa wengine wakati mie kanipa wali mtupu" hapa anaonekana mchezaji Nyemo John Chinyabe akiwaza kwa mshangao. wagogo kwa nyama!!
Leonard Richard, Shaabani Machumane na Wetson Mwamafupa wakisikiliza maneno ya busara kutoka kwa wawakilishi wa Mbeya Veterans baada ya kumalizika kwa mchezo kirafiki baina yao wakati wa sherehe za pasaka 2010.
Vikosi mchanganyiko Mbeya Veterans na Segerea Veterans wakati wa bananza la pasaka 2010 huko segerea dar es salaam
beki Ayawi Daraja akitafuta namna ya kupiga chenga shambuliaji moja la Buguruni, bonge la mtu. ngoja tutamuuliza kama alifanikiwa kupiga chenga.
Anaitwa Haule beki wa Segerea Veterans akianua kinu juani kuepuka lawama dhidi ya wachezaji watatu wa Buguruni Veterans wakati wa bonanza segerea wakati wa pasaka 2010.
wanamwita Ngassa wa Segerea Veterans, hapa Mh: Ally Katembo akimnyanyasa beki wa Mbeya Veterans kwa chenga za maudhi na kutoa pasi kama za Gaucho.

Hatuna hakika kama hapa Kibona alipitwa ama laa. Kwani huyu jamaa labda upite mpira peke yake ama mchezaji peke yake, kupita vyote ni ngumu sana. wanaume kazini Segerea Veterans na Buguruni Veterans wakati wa Pasaka 2010.
Timu kamambe ya Mbeya Veterans (Mbalizi) baadhi ya wachezaji ni kama Shaaban kiungo wa zamani wa Majimaji wapili kushto waliosimama na Ephraim Kayeta mshambuliaji mwenye akili, kasi na mashuti wa timu za Mecco ya Mbeya na timu ya taifa ya tTanzania enzi hizokatikati waliosimama. hapa ni kabla ya pambano lao na timu ya Buguruni Veterans wakati wa pasaka 2010. Wengine pichani ni jairo, mwasa, kaunda na wengineo.
Kutoka kushoto waliosimama ni Mwalimu Wandawanda, Karume Uledi, Gaydon Mtenga, Mganga Laurian, Khalid Oming'o, Shaaban Machumane, Ayawi Ally Daraja, Ephraim Makoye, Mao Mkami (Ball Dancer) Mh: Ramadhani Maleta, Airform Kibona,Muhidini Sisso na Spear Mbwembwe. Waliochuchumaa kutoka kushoto ni Nyemo John Chinyabe (Berbatov) Leonard Richard Mwakasege (Zidane) Mohameid "Kukovic" Mh: Ally Katembo, Mohameid Diego, Salum Mwamtuya (Baba Said) na Eliud Pemba. Hiki ndio kikosi kamili cha Segerea Veterans kilichopambana na timu za Mbalizi Veterans na Buguruni Veterans wakati wa sherehe za pasaka 2010.
Kutoka kushoto Mh: Ally Katembo, Khalid Oming'o, Mh: Ramadhani Maleta, Gaydon Mtenga,Mganga Laurian na Muhidini Sisso wakipasha kuwakabili Buguruni Veterans siku ya PASAKA 6/4/2010
Baadhi ya wachezaji wa Mbalizi Veterans kutoka Mbeya wakipiga jaramba kabla ya kuikabili timu ya Segerea Veterans