Monday, October 22, 2012

apa marehemu Oming'o alikuwa anafuatilia kwa karibu mpambano uliokuwa ukipigwa kati ya Segerea na Mburahati Veterans.
Jacob Aridi - Oming'o (aliyejishika kiunoni) alikuwa ni shabiki nambari moja wa Simba na Liverpool, hapa ilikuwa ni ktk mpambano wa mashabiki wa simba na wale wa Yanga.. siku zote palikuwa panachimbika. tutakukosa mno kamanda na rafiki wa kweli. Pumziko la Amani ulipate na raha milele utapewa na mwanga wa milele utaangaziwa.
Marehemu Jacob Odhiambo Aridi- Oming'o alikuwa daima ni mcheshi na mtu alokuwa mstari wa mbele kulisogeza mbele gurudumu la segerea veterans, hapa ilikuwa ni mitaa ya mburahati. Pumzika kwa Amani
TANZIA
Wana Segerea Veterans and Social Club wanasikitika kutangaza kifo cha mchezaji mwenzetu, Jacob Othiambo Aridi, al-maaruf kama Oming'o ( aliyeruka juu akiwa na jezi ya barcelona) kilichotokea akiwa anafanja mechi mazoezi pamoja na timu za Moro United na Segerea Veterans siku ya jumamosi tarehe 19/10/2012 saa 2.30 asubuhi katika uwanja wa Toto Tundu Segerea, juhudi zote za kunususru maisha ya marehemu Oming'o zilifanyika lakini mapenzi ya Mungu yaheshimiwe. Mwili wa marehemu Oming'o utaagwa nyumbani kwake Segerea Sanene siku ya jumanne tarehe 23/10/2012 kuanzia saa 9.00 alasiri na kusafirishwa kesho yake kuelekea Rorya Mara kwa mazishi. TUTAKUKUMBUKA DAIMA.