Monday, October 22, 2012

TANZIA
Wana Segerea Veterans and Social Club wanasikitika kutangaza kifo cha mchezaji mwenzetu, Jacob Othiambo Aridi, al-maaruf kama Oming'o ( aliyeruka juu akiwa na jezi ya barcelona) kilichotokea akiwa anafanja mechi mazoezi pamoja na timu za Moro United na Segerea Veterans siku ya jumamosi tarehe 19/10/2012 saa 2.30 asubuhi katika uwanja wa Toto Tundu Segerea, juhudi zote za kunususru maisha ya marehemu Oming'o zilifanyika lakini mapenzi ya Mungu yaheshimiwe. Mwili wa marehemu Oming'o utaagwa nyumbani kwake Segerea Sanene siku ya jumanne tarehe 23/10/2012 kuanzia saa 9.00 alasiri na kusafirishwa kesho yake kuelekea Rorya Mara kwa mazishi. TUTAKUKUMBUKA DAIMA.

No comments:

Post a Comment