Tuesday, February 23, 2010

Timu ya Segerea Veterans siku ya jumapili tarehe 21/02/2010 ilitoa dozi kali kwa timu ya Buguruni Combine Veterans kwa kipigo cha magoli 3-2 magoli yakiwa yamewekwa kimiani na Airform Kibona (penati dk ya 15), Ally Ruvu mchezaji wa zamani wa timu za Simba Sports Club na JKT Ruvu na Karume (Mmanyema). Nyota ya mchezo alikuwa ni Mao Mkami (Ball Dancer) mkali wa zamani watimu za TP Lindanda Pamba (wana kawekamo) ya Mwanza na timu za Mtibwa na Manyema. Jamaa huwezi amini, yupo sawa kama alivyo kuwa enzi hizo akiwalisha mipira kina Fumo Felician, Kitwana Selemani, Beya Simba, Hussein Marsha na wakali wengine wa TP Lindanda. Still dancing with a ball as he was doing decades ago, bravo pal.

No comments:

Post a Comment