Monday, February 8, 2010

jana jumapili tarehe 6/2/2010 timu kabambe ya Segerea Veterans ilikuwa na mpambano wa kirafiki baina yake na timu machachari ya Mbezi Beach Veterens iliyo chini ya ufadhili na udhamini wa Giraffe Hotel.

Katika mchezo huo matokeo yalikuwa Segerea Veterans 2 na Mbezi Beach Veterans 1 (SVSC 2- MBVSC 1) magoli ya Segerea yaliwekwa kimiani na mchezaji wa zamani wa simba na yanga Ephraim Makoye katika dakika ya 7 na Karume dakika ya 30 kipindi cha pili na lile la Mbezi Beach liliwekwa kimiani na mchezaji wa zamani wa Ushirika Moshi Hashimu. (picha zitafuata baadae)

Timu ya Segerea ilicheza mchezo wa kufurahisha kiasi cha kuwaduwaza wapinzani wao muda wote wa mchezo. Kiungo mahili wa Taifa stars na mchezaji wa timu za Vijana Ilala (Kabaka yeka) na Mtibwa Sugar Hussin Sweddy aling'arisha vilivyo katikati, huku Zidane (Richard) akiikosesha timu yake ya Segerea Veterans magoli kadhaa ya wazi. Nyota ya mchezo kwa mujibu wa Mbezi Beach Veterans alikuwa ni mlinda mlango wa Segerea Veterans Mustafa "Kukovic"


Katika hatua nyingine Timu za Segerea Veterans na Mbezi Beach zinajiandaa kuipokea timu ya Mbeya Veterans siku ya jumamosi ya Pasaka na PASAKA KUU katika mabonanza yatakayo fanyika Mbzi Beach na Segerea. Timu ya Mbeya inayoundwa na wakali wa timu za Tukuyu Stars (Banyambala) na Mecco chini ya uongozi wakali kama charles Makwaza, na wengineo inatarajiwa kuwasili jijini siku ya ijumaa kuu.

Taarifa zaidi juu ya timu za Iringa na Ruvuma zitatolewa hapo baadae.

No comments:

Post a Comment