Tuesday, October 19, 2010
Monday, October 18, 2010
Sunday, October 17, 2010
Saturday, October 9, 2010
Monday, August 16, 2010
Mwalimu Spear Mbwembwe akiongoza sebene la Twanga pepeta huku wachezaji wake wa segerea veterans Aleche Ninje, Emmanuel Kazimoto, Leonard Richard na Othman Katembo wakiserebuka kwa chati uwanja wa Jamhuri Morogoro wakati wa tamasha la nanenane kabla ya kupambana na Tanzania Stars chini ya Juma Mkambi 'General'
Friday, June 18, 2010
Monday, May 24, 2010

"the Special One" kutua Segerea Veterans.
Homa imeanza kuwapanda waalimu ya timu ya Segerea Veterans kuwa yule kocha mwenye mafanikio na mbwembwe nyingi kipenzi cha watu, kiboko wa wote wenye akili Jose Mourinho yupo mbioni kukamilisha mkataba wa siku kumi kukinoa kikosi hicho. aaaaaaaahhh, utani tu jamani.

Friday, April 9, 2010
Monday, March 22, 2010
TANZIA
Uongozi na wanachama wa Segerea Veterans Sports Club wanasikitika kutangaza kifo cha mwanachama mwenzao wa Hiyari ambaye pia ni mke mkubwa wa Senior Member Chief Uyeka Idd Lumbyambya Mavanga wa pili kilichotokea siku ya jumamosi tarehe 20/3/2010 na mazishi kufanyika siku hiyo hiyo katika makaburi ya Kichifu huko Segerea. (Innah hillah Raajun)
Tulimpenda saana shemeji yetu, lakini Allah amempenda zaidi. Amin.

Tuesday, February 23, 2010
Timu ya Segerea Veterans siku ya jumapili tarehe 21/02/2010 ilitoa dozi kali kwa timu ya Buguruni Combine Veterans kwa kipigo cha magoli 3-2 magoli yakiwa yamewekwa kimiani na Airform Kibona (penati dk ya 15), Ally Ruvu mchezaji wa zamani wa timu za Simba Sports Club na JKT Ruvu na Karume (Mmanyema). Nyota ya mchezo alikuwa ni Mao Mkami (Ball Dancer) mkali wa zamani watimu za TP Lindanda Pamba (wana kawekamo) ya Mwanza na timu za Mtibwa na Manyema. Jamaa huwezi amini, yupo sawa kama alivyo kuwa enzi hizo akiwalisha mipira kina Fumo Felician, Kitwana Selemani, Beya Simba, Hussein Marsha na wakali wengine wa TP Lindanda. Still dancing with a ball as he was doing decades ago, bravo pal.
Saturday, February 13, 2010

Tunatamani kama angekuwa bado anacheza soka ya upinzani labda angeweza kutupa miaka ya sasa. Ukitaka kuona vitu vyake watafute Segerea Veterans wanapocheza, haiitaji kuambiwa utaona beki akiwanyanyasa washambuliaji utajua tu huyo ndiye Salum Mwantuya.
Wednesday, February 10, 2010
Monday, February 8, 2010
jana jumapili tarehe 6/2/2010 timu kabambe ya Segerea Veterans ilikuwa na mpambano wa kirafiki baina yake na timu machachari ya Mbezi Beach Veterens iliyo chini ya ufadhili na udhamini wa Giraffe Hotel.
Katika mchezo huo matokeo yalikuwa Segerea Veterans 2 na Mbezi Beach Veterans 1 (SVSC 2- MBVSC 1) magoli ya Segerea yaliwekwa kimiani na mchezaji wa zamani wa simba na yanga Ephraim Makoye katika dakika ya 7 na Karume dakika ya 30 kipindi cha pili na lile la Mbezi Beach liliwekwa kimiani na mchezaji wa zamani wa Ushirika Moshi Hashimu. (picha zitafuata baadae)
Timu ya Segerea ilicheza mchezo wa kufurahisha kiasi cha kuwaduwaza wapinzani wao muda wote wa mchezo. Kiungo mahili wa Taifa stars na mchezaji wa timu za Vijana Ilala (Kabaka yeka) na Mtibwa Sugar Hussin Sweddy aling'arisha vilivyo katikati, huku Zidane (Richard) akiikosesha timu yake ya Segerea Veterans magoli kadhaa ya wazi. Nyota ya mchezo kwa mujibu wa Mbezi Beach Veterans alikuwa ni mlinda mlango wa Segerea Veterans Mustafa "Kukovic"
Katika hatua nyingine Timu za Segerea Veterans na Mbezi Beach zinajiandaa kuipokea timu ya Mbeya Veterans siku ya jumamosi ya Pasaka na PASAKA KUU katika mabonanza yatakayo fanyika Mbzi Beach na Segerea. Timu ya Mbeya inayoundwa na wakali wa timu za Tukuyu Stars (Banyambala) na Mecco chini ya uongozi wakali kama charles Makwaza, na wengineo inatarajiwa kuwasili jijini siku ya ijumaa kuu.
Taarifa zaidi juu ya timu za Iringa na Ruvuma zitatolewa hapo baadae.

Thursday, January 28, 2010

, Mashaka, Haule
Toleo la vikosi mbalimbali vya Segerea Veterans, hapa ni siku ya kumbukumbu ya Rais wetu marehemu Mperemba. Kutoka kushto waliosimama ni Martin Richard Tupilike, Bilary, Andrew Ng'ong'a (Nigeria) Chifu Uyeka Idd Lumbyambya Mavanga wa II (Chifu wa Wanyiha na makabila yote madgo mkoa wa Mbeya), Richard Mwakasege (Zidane) na Gaydon Mtenga.
Waliinama kutoka kushoto ni Othman Katembo, Emmanuel Kazimoto (Baba Glory- mkwe) Airform Kibona, Mashaka, Haule, Herry Kisiki, Godfrey na Ernest.

Waliinama kutoka kushoto ni Othman Katembo, Emmanuel Kazimoto (Baba Glory- mkwe) Airform Kibona, Mashaka, Haule, Herry Kisiki, Godfrey na Ernest.

Waliopiga goti toka kushoto ni Bilary,Karume,Babu Ayawi, Herry Kisiki, Mashaka, Airform Kibona na Yackub (Cisse) aliyelala ni Godfrey.
Subscribe to:
Posts (Atom)