Tuesday, February 23, 2010
Timu ya Segerea Veterans siku ya jumapili tarehe 21/02/2010 ilitoa dozi kali kwa timu ya Buguruni Combine Veterans kwa kipigo cha magoli 3-2 magoli yakiwa yamewekwa kimiani na Airform Kibona (penati dk ya 15), Ally Ruvu mchezaji wa zamani wa timu za Simba Sports Club na JKT Ruvu na Karume (Mmanyema). Nyota ya mchezo alikuwa ni Mao Mkami (Ball Dancer) mkali wa zamani watimu za TP Lindanda Pamba (wana kawekamo) ya Mwanza na timu za Mtibwa na Manyema. Jamaa huwezi amini, yupo sawa kama alivyo kuwa enzi hizo akiwalisha mipira kina Fumo Felician, Kitwana Selemani, Beya Simba, Hussein Marsha na wakali wengine wa TP Lindanda. Still dancing with a ball as he was doing decades ago, bravo pal.
Saturday, February 13, 2010
Mheshimiwa Ally Katembo akichangia mawaidha ya busara na Ndugu zetu wa Boko Veterans. Jamaa walimwaga unywaji si mchezo, hapa anaonekana Mheshimiwa Boli Zozo akikubaliana na mawazo ya Mheshimiwa Katembo kwa kutikisa chupa ya ulabu, wengine pichani ni Muhudini Sisso, Spear Mbwembwe na Juma Katembo mwenye chupa ya maji Uhai.
Beki aliyerudi katika kiwango cha zamani ambaye alikuwa nyota ya Tabora na watu kama Ally Mayai, Huruna Moshi, Idd Moshi, Mrisho Moshi, Mohamed Banka, Yahya Akilimali walikuwa wanajifunza mavitu kutoka kwake Salum Mwamtuya (Baba Said).
Tunatamani kama angekuwa bado anacheza soka ya upinzani labda angeweza kutupa miaka ya sasa. Ukitaka kuona vitu vyake watafute Segerea Veterans wanapocheza, haiitaji kuambiwa utaona beki akiwanyanyasa washambuliaji utajua tu huyo ndiye Salum Mwantuya.

Wednesday, February 10, 2010
Monday, February 8, 2010
jana jumapili tarehe 6/2/2010 timu kabambe ya Segerea Veterans ilikuwa na mpambano wa kirafiki baina yake na timu machachari ya Mbezi Beach Veterens iliyo chini ya ufadhili na udhamini wa Giraffe Hotel.
Katika mchezo huo matokeo yalikuwa Segerea Veterans 2 na Mbezi Beach Veterans 1 (SVSC 2- MBVSC 1) magoli ya Segerea yaliwekwa kimiani na mchezaji wa zamani wa simba na yanga Ephraim Makoye katika dakika ya 7 na Karume dakika ya 30 kipindi cha pili na lile la Mbezi Beach liliwekwa kimiani na mchezaji wa zamani wa Ushirika Moshi Hashimu. (picha zitafuata baadae)
Timu ya Segerea ilicheza mchezo wa kufurahisha kiasi cha kuwaduwaza wapinzani wao muda wote wa mchezo. Kiungo mahili wa Taifa stars na mchezaji wa timu za Vijana Ilala (Kabaka yeka) na Mtibwa Sugar Hussin Sweddy aling'arisha vilivyo katikati, huku Zidane (Richard) akiikosesha timu yake ya Segerea Veterans magoli kadhaa ya wazi. Nyota ya mchezo kwa mujibu wa Mbezi Beach Veterans alikuwa ni mlinda mlango wa Segerea Veterans Mustafa "Kukovic"
Katika hatua nyingine Timu za Segerea Veterans na Mbezi Beach zinajiandaa kuipokea timu ya Mbeya Veterans siku ya jumamosi ya Pasaka na PASAKA KUU katika mabonanza yatakayo fanyika Mbzi Beach na Segerea. Timu ya Mbeya inayoundwa na wakali wa timu za Tukuyu Stars (Banyambala) na Mecco chini ya uongozi wakali kama charles Makwaza, na wengineo inatarajiwa kuwasili jijini siku ya ijumaa kuu.
Taarifa zaidi juu ya timu za Iringa na Ruvuma zitatolewa hapo baadae.

Subscribe to:
Posts (Atom)